X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 17/Feb 16:50

TANZANIA KUHUDUMIA NCHI 14 NISHATI YA MAFUTA

Na Denis Chambi , Tanga.SERIKALI imeanza  mchakato wa uboreshaji wa miundombinu ya Bomba la Tazama  linalosafirisha mafuta kutoka Tanzania hadi Zambia lengo likiwa ni kuongeza nchi zinazotumia huduma hiyo kutoka nchi 12 kwa sasa  hadi 14.Hayo yameelezwa  February 17, 2025 na Naibu waziri Mkuu ambaye pia ni waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko wakati akifungua  kikao cha 4 cha Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji " EWURA" Kilichofanyika Mkoani Tanga ambapo amesema kuwa uhitaji wa mafuta hapa nchini umeongezeka tofauti na awali. Dkt. Biteko amesema kuwa Bomba hilo lililojengwa mwaka 1970  likiwa linatembea zaidi ya Kilomita 1,700 limekuwa halina vituo vya kushushia mafuta kwa muda mrefu na kupelekea msongamano wa magari katika bandari ya Dar es salaam hivyo Serikali imeamua pamoja na maboresho yatakayofanyika kujenga vituo mbalimbali hapa nchini.Alisema moja wapo ya maeneo ambayo yatajengwa vituo hivyo ni Makambako Mkoani Mbeya pamoja na Morogoro ambapo vitarahisisha  usafirishaji wa Nishati hiyo pamoja na kuondoa mianya ya rushwa huku akibinisha kuwa bado Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na Uganda kupitia mradi wa EACOP."Leo nishati Duniani ni  hitaji kubwa sasa hivi tuna bomba letu la Tazama linalopeleka mafuta Zambia limejengwa miaka ya 1970 mahitaji ya mafuta Zambia na sisi ndani  yamekuwa makubwa tunataka kulipanua kulitoa kwenye nchi 12 zilizopo hadi 14 tusingependa kuwa na Bomba ambalo linatembea zaidi ya Kilomita 1,700 bila ya kuwa na matank njiani" "Nia yetu ni kwamba tuondoe foleni  ya magari Dar es salaam yanayokuja kuchukua mafuta bandarini na kutengeneza msongamano tunataka mafuta ya Mbeya yachukuliwe Makambako na Morogoro bado tuna mazungumzo na watu wa Uganda Awali akizungumza mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi na  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na maji 'EWURA' Dkt. James Andelile  alisema kuwa wameendelea kuhamasisha uwekezaji wa Nishati kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje."EWURA imejenga mazingira wezeshi kwaajili ya uwekezaji hapa nchini kwa viwango vya ufanisi kuanzia November hadi December 2024 tumetoa vibali 8 na  wawekezaji takribani hamsini ambao wameonyesha nia ya kuwekeza wakishamalizana na TPDC tutatoa vibali kwa wakati" alisema Dkt Andelile Alisema EWURA imetekeleza maagizo ya kufikisha huduma ya Nishati ya mafuta mpaka vijijini iliyotolewa na Dkt Biteko ambapo imeweza kupunguza gharama za vibali kutoka shilingi  laki Tano '500,000' hadi elfu hamsini '50,000'  pamoja na kupunguza maombi ya leseni kutoka Milioni moja '1,000,000' hadi shilingi  laki moja '100,000'."Agizo ambalo ulilitoa la kuwezesha ujenzi wa vituo  vya kuuza mafuta  katika maeneo ya vijiji mbalimbali na kupunguza masharti ya ujenzi wa mafuta ikiwemo kupunguza gharama za vibali kutoka laki Tano hadi shilingi elfu hamsini na kupunguza maombi ya leseni  kutoka Milioni moja mpaka laki moja tumeendelea kufanya mawasiliano na REA ili kuhakikisha vituo vingi vinajengwa vijijini na kurahisisha upatikanaji wa Nishati safi katika hali ya usalama" alisema.Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani alisema kuwa Serikali imetoa kiasi cha  shilingi  Trillion  3.60 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya  usambazaji wa umeme ambapo tayari vijiji 763 vimefikiwa na huduma hiyo  pamoja na vitongoji 4,596 ikiwa ni sawa na asilimia 50." Sisi katika Mkoa wetu wa Tanga tumepata kiasi cha shilingi Trillion 3.60 ambazo zimeelekezwa katika miradi mbalimbali na tumefanikiwa kupeleka umeme  katika vijiji vyote 763 na kasi ya kupeleka umeme katika vitongoji vyetu 4,596 si kazi kubwa sana lengo ni kuhakikisha tunavifikia vitongoji vyote.Alisema katika kutokomeza matumizi ya kuni na mkaa na kuhamia  kwenye matumizi ya Nishati safi  Mkoa umeendelea kuzisimamia taasisi zenye watu zaidi ya 100 ikiwa ni maelekezo ya Serikali ambapo mpaka sasa taasisi 1493 zimeshakaguliwa huku wananchi zaidi ya 735,372 kati ya 2,600,000 wanatumia Nishati safi na salama. 

Articles similaires

BARRICK YACHANGIA SHILINGI TRILIONI 3.6 PATO LA SERIKALI KWA KIPINDI CHA MIAKA 4

msumbanews.co.tz - 14/Feb 08:44

Meneja wa Barrick nchini, Dk.Melkiory Ngido akitoa taarifa ya utendaji wa Barrick na Twiga kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na...

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 16,275 MKOANI SIMIYU

msumbanews.co.tz - 19/Feb 05:42

 🎈🎈Mitungi 3,255 yaanza kusambazwa wilayani MaswaMkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenani Kihongosi, leo tarehe 18 Februari, 2025 amezindua rasmi...

BARRICK YACHANGIA SHILINGI TRILIONI 3.6 SERIKALINI KWA KIPINDI CHA MIAKA MINNE

msumbanews.co.tz - 14/Feb 04:23

 • Yachangia Zaidi ya Shilingi Trilioni 11 katika Uchumi wa Tanzania• Gawio la Zaidi ya Shilingi Bilioni 412 latolewa kwa SerikaliKampuni ya...

DKT.BITEKO AIPONGEZA EWURA KULETA UTULIVU KWENYE NISHATI

msumbanews.co.tz - 17/Feb 15:54

  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko,akizungumza wakati akifungua kikao cha nne cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa...

BARRICK NI KIELELEZO BORA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI NCHINI- DKT. KIRUSWA

msumbanews.co.tz - 16/Feb 06:20

 • Kamati ya Bunge Yataka Kampuni Zingine Kuiga Barrick📍 KahamaNaibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema kuwa Kampuni ya Uchimbaji wa...

ULEGA ATAKA WATAALAMU WAKUNE VICHWA KUONDOA KERO YA FOLENI MIJINI

msumbanews.co.tz - 13/Feb 18:11

 WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka wataalamu wa wizara hiyo kutumia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mkoani Singida kubuni njia...

TANZANIA YAPONGEZWA KWA UKUAJI MZURI WA UCHUMI NA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU

msumbanews.co.tz - 21/Feb 19:23

 Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, DodomaWashirika wa Maendeleo nchini wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa maendeleo mbalimbali hususan...

WAFUNGWA KUANZA KUPEWA UJUZI GEREZANI NA VYETI VINAVYOTAMBULIWA NA VETA: BASHUNGWA

msumbanews.co.tz - 15/Feb 07:49

 📍Azindua Mabasi ya kusafirisha MaabusuWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innnocent Bashungwa amelitaka Jeshi la Magereza kusimamia kikamilifu...

JENGO LA HAZINA - GEITA LAZINDULIWA

msumbanews.co.tz - 18/Feb 07:15

 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo (Mb), amezindua rasmi Jengo la Hazina Mkoa wa Geita kwa...

SERIKALI YAJIDHATITI KUBORESHA SEKTA YA KILIMO – DKT BITEKO

msumbanews.co.tz - 14/Feb 09:02

 📌 Anadi soko la mazao jamii ya mikunde India📌 Mnada mazao ya kunde mtandaoni waboresha biashara ya kimataifa📌 Biashara kati ya Tanzania na...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément