X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 06/Sep 09:36

BARAZA LA MADIWANI WALAANI MAUAJI YA WATU SABA.

Na, Elizabeth Paulo; Dodoma Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Chemba limelaani vikali kitendo kilichotokea hivi karibuni la Mganga wa Kienyeji aliyetuhumiwa kwa mauaji mkoani Singida na mji mwingine Wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma ambako yamebainika mashimo sita walimozikwa watu.Akizungumza Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Chemba Saidi Sambala katika kikao cha Baraza la Madiwani amesema wanalipongeza jeshi la polisi kwa kufanya upelelezi na kubaini jumla ya miili ya watu 10 waliouawa.Katika Taarifa iliyotolewa Agosti 26,2024 na msemaji wa Jeshi la polisi, David Misime imesema katika mwendelezo wa uchunguzi wamebaini miili ya watu 10  waliouawa kati ya hiyo mitatu ilipatikana Mkoani Singida na Dodoma ilipatikana saba .Kati ya Miili hiyo, Amesema mmoja ulitupwa porini na mingine tisa ilizikwa kwa kukalishwa kwenye shimo kwa namna wahisika walivyosukumwa na imani zao  za kishirikina.Aidha Jeshi la polisi linatoa woto kwa Wananc0hi kuendelea kutoa taarifa za kweli na Sahihi na kuendelea kukemea kuanzia ngazi ya familia ili kuzuia na kukomesha vitendom vinavyoendelea kutokea ndani ya Jamii kwa Siri kubwa .Wakizungumza  mara baada ya kikao cha Baraza baadhi ya Madiwani wameiomba Jeshi la Polisi  kuendelea kuisaidia jamii kwa kuendeleza uchunguzi wa matukio mbalimbali kama yalivyotokea Dodoma na Singida ili kubaini watu wengine wanaotekeleza uhalifu.Aidha wamesema hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Articles similaires

POLISI WAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA CHADEMA ,CCM WALAANI UTEKAJI

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:02

Jeshi la polisi nchini Tanzania limepiga marufuku maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama cha upinzani Chadema kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe...

WAZIRI RIDHIWANI APONGEZA BARAZA LA LESCO KWA UTENDAJI MZURI

msumbanews.co.tz - 06/Sep 04:47

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amepongeza Baraza la Ushauri wa Masuala ya...

MAGARI YENYE MFUMO MBOVU WA BREKI YAKAMATWA MKOANI SONGWE

msumbanews.co.tz - 18/Sep 07:03

Wamiliki wa vyombo vya moto nchini wametakiwa kuhakikisha Madereva wa vyombo hivyo wanafuata sheria za usalama barabarani na kuacha mara moja tabia ya...

MAGARI YENYE MFUMO MBOVU WA BREKI YAKAMATWA MKOANI SONGWE

msumbanews.co.tz - 18/Sep 07:03

Wamiliki wa vyombo vya moto nchini wametakiwa kuhakikisha Madereva wa vyombo hivyo wanafuata sheria za usalama barabarani na kuacha mara moja tabia ya...

WAZIRI CHANA " SERIKALI ITAWALINDA WANANCHI DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI"

msumbanews.co.tz - 06/Sep 17:20

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka  mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...

WAZIRI CHANA " SERIKALI ITAWALINDA WANANCHI DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI"

msumbanews.co.tz - 06/Sep 17:20

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka  mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...

NGORONGORO WANAIPENDA CCM NA NI NGOME YA CCM

msumbanews.co.tz - 07/Sep 07:46

 KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, amesema Ngorongoro ni ngome ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hakuna chama...

WATUMIA SHEREHE ZA UBATIZO KUKEKETA WATOTO SERIKALI YAONYA

msumbanews.co.tz - 17/Sep 09:34

Baadhi ya familia za Jamii ya kimasai wilaya ya Longido mkoa Arusha,zinadaiwa kutumia sherehe za Ubalozi kukeketa watoto wadogo ili kukwepa kukamatwa...

MSIUZE MAENEO YA WAZI - PINDA

msumbanews.co.tz - 18:34

  Na Mwandishi Wetu, Moshi Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewataka Watanzania kuacha mara moja tabia ya...

WAZIRI JAFO SERIKALI IMEWEKA MAZINGIRA MAZURI YA KUFANYA BIASHARA,AAGIZA UJENZI VIWANDA 30

msumbanews.co.tz - 12/Sep 05:38

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dk.Selemani Jafo amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufanyia biashara kwa kufanya uwekezaji ikiwa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément