Na. Saidina Msangi, Kibaha, Pwani.Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau na Taasisi zilizo chini yake imejipanga kutoa elimu ya fedha kwa...
Vous n'êtes pas connecté
Na. Saidina Msangi, Chalinze, Pwani.Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia elimu ya fedha itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi kwa kutumia fursa za uwekezaji ili kujiongezea kipato na kuongeza thamani ya akiba zao.Wananchi hao walitoa shukrani hizo baada ya kupata mafunzo ya elimu ya fedha yaliyoratibiwa na Wizara ya Fedha, yenye kauli mbiu "Elimu ya fedha ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi" ambayo yametolewa kwa siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa Wilaya ya Halmashauri ya Chalinze. Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake, Bi. Mery Leonard Chiwiko, aliishukuru Wizara ya Fedha kwa kuwapa elimu hiyo muhimu, akisema kuwa hapo awali hawakuwa na uelewa mzuri kuhusu masuala ya fedha, mikopo na uwekezaji."Tunaishukuru Wizara ya Fedha kwa kutupatia elimu hii, itatusaidia sana katika kuimarisha maisha yetu ya kifedha, kuepukana na mikopo umiza na pia tumejifunza kuwa hata kama una kipato kidogo inawezekana kuweka akiba na kuwekeza akiba hiyo na kupata faida," alisema Chiwiko.Wananchi hao waliiomba Serikali kuona namna ya kuwafikishia mafunzo ya elimu ya fedha ikiwezekana mara mbili kwa mwaka kutokana na umuhimu wake katika kuwawezesha kukabiliana na changamoto za kiuchumi.Timu ya Maafisa kutoka kutoka Wizara ya Fedha imetoa mafunzo ya elimu ya fedha ikiwemo namna ya kuweka akiba na mbinu za usimamizi wa fedha na uwekezaji kwa washiriki zaidi ya 800 ambao wanatarajiwa kuwa mabalozi wa kuwafikishia wenzao elimu hiyo ili nao waweze kunufaika na kujikwamua kiuchumi.
Na. Saidina Msangi, Kibaha, Pwani.Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau na Taasisi zilizo chini yake imejipanga kutoa elimu ya fedha kwa...
Na. Saidina Msangi, Mkuranga Pwani.Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, imewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa...
Na. Saidina Msangi, WF, Bagamoyo, Pwani.Watumishi na wananchi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wameishukuru Serikali kwa kuwapa mafunzo ya elimu...
Na Mwamvua Mwinyi,KibahaWIZARA ya fedha imetoa rai kwa Watanzania hususan makundi ya akinamama na wajasiriamali kujiepusha na mikopo ya...
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Abdul Mhinte akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa wataalamu kutoka...
Na Chedaiwe Msuya, WF.Wizara ya Fedha inaendelea kutoa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta...
Na Chedaiwe Msuya,WFWizara ya Fedha imehitimisha utoaji wa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi kwa Umma katika mikoa ya Mtwara, Lindi na...
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde amezipongeza Kampuni za uzalishaji wa makaa ya mawe kwa kuongeza uzalishaji na kuzitaka kuelekeza zaidi...
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo Septemba 12 ,2024 ameendelea na ziara ya kutatua kero za Wananchi wa Kata za Kitunda, Kivule, Mzinga...
Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa ,Kitila Mkumbo akizngumza wakati akifungua Wiki ya AZAKI iliyoanza rasmi leo Septemba 9-13, 2024 Jijini...