X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 09/Sep 07:12

WANANCHI BAGAMOYO WAPOKEA ELIMU YA FEDHA

 Na. Saidina Msangi, WF, Bagamoyo, Pwani.Watumishi na wananchi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wameishukuru Serikali kwa kuwapa mafunzo ya elimu ya fedha yanayotolewa na Wizara ya Fedha kwa kuwa yamewafungua na kuwapa mwanga wa kujiandaa kustaafu wakiwa na uchumi imara.Walitoa shukrani hizo kwa nyakati tofauti Mjini Bagamoyo, mkoani Pwani, baada ya mafunzo ya siku mbili yaliyotolewa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha ukihusisha watumishi katika ukumbi wa mikutano wa wilaya, na wananchi katika ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, (TaSUBa).Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zuwena Ungele, alisema kuwa elimu ya fedha waliyoipata imewapa motisha ya kuanza kujiandaa na maisha ya kustaafu.‘’Sisi ni mabalozi wa watumishi wa Serikali kwa ujumla sasa unapostaafu ukawa na maisha mabaya unaleta picha mbaya kuwa unaweza kuwa mtumishi wa Serikali unastaafu ukiwa umechoka kimaisha hivyo tujipange kulinda taswira ya Serikali kwa kujiandaa kustaafu tukiwa imara kiuchumi’’, alisema Bi. Ungele.Alisisitiza kuwa watumishi ni wastaafu watarajiwa hivyo ni vema kuanza kuweka mpango na maandalizi ya kustaafu mapema ili wakati ukifika wawe na akiba ya kuwawezesha kuishi Maisha yenye hadhi.Aidha, wameishukuru Wizara kwa elimu ya fedha na kutoa rai kuwa elimu hiyo itolewe mara kwa mara ili iwe chachu ya kuhamasisha watumishi na wananchi kwa ujumla kujenga utaratibu wa kujiandaa na maisha ya kustaafu.Akizungumza wakati akitoa elimu kwa watumishi na wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo, Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya alisema kuwa Serikali inatekeleza programu ya utoaji wa elimu ya fedha kwa wananchi ili kuhakikisha kuwa wanapata elimu ya fedha ya kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi kuhusu fedha zao.‘‘Ni lazima kuwa makini sana katika kupanga matumizi ya fedha, hakikisha unasimamia mapato na matumizi, matumizi yasizidi mapato, kila fedha unayopata tunza asilimia kumi tuwe na utaratibu wa kuweka akiba katika sehemu rasmi kwani akiba haiozi na kuhakikisha kuwa unapochukua mikopo taasisi hiyo imesajiliwa na ina leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania,’’ alisisitiza Bw. Kibakaya.

Articles similaires

WANANCHI CHALINZE WAJIPANGA KUWEKEZA

msumbanews.co.tz - 07/Sep 07:41

 Na. Saidina Msangi, Chalinze, Pwani.Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia elimu ya fedha...

WATANZANIA ASILIMIA 80 KUFIKIWA NA ELIMU YA FEDHA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 05:24

 Na. Saidina Msangi, Kibaha, Pwani.Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau na Taasisi zilizo chini yake imejipanga kutoa elimu ya fedha kwa...

WAZIRI MAVUNDE AYATAKA MAKAMPUNI YA MAKAA YA MAWE KUWEKEZA KATIKA UZALISHAJI WA UMEME

msumbanews.co.tz - 17/Sep 05:17

Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde amezipongeza Kampuni za uzalishaji wa makaa ya mawe kwa kuongeza uzalishaji na kuzitaka kuelekeza zaidi...

WIZARA YA FEDHA YAKEMEA MIKOPO HOLELA YA MITAANI INAYODHALILISHA WATANZANIA

msumbanews.co.tz - 12/Sep 07:52

 Na Mwamvua Mwinyi,KibahaWIZARA ya fedha imetoa rai kwa Watanzania hususan makundi ya akinamama na wajasiriamali kujiepusha na mikopo ya...

ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WANANCHI WA MKURANGA

msumbanews.co.tz - 11/Sep 05:10

 Na. Saidina Msangi, Mkuranga Pwani.Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, imewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa...

WIZARA YA FEDHA IMEHITIMISHA KUTOA MAFUNZO YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA KANDA YA KUSINI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:55

 Na Chedaiwe Msuya,WFWizara  ya Fedha imehitimisha utoaji wa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi kwa Umma  katika mikoa ya Mtwara, Lindi na...

WAZIRI CHANA " SERIKALI ITAWALINDA WANANCHI DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI"

msumbanews.co.tz - 06/Sep 17:20

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka  mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...

WAZIRI CHANA " SERIKALI ITAWALINDA WANANCHI DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI"

msumbanews.co.tz - 06/Sep 17:20

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali itaendelea kuweka  mikakati madhubuti za kuwalinda wananchi...

WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO KWA MAAFISA UNUNUZI WA TAASISI ZA UMMA.

msumbanews.co.tz - 06/Sep 04:51

 Na Chedaiwe Msuya, WF.Wizara ya Fedha inaendelea kutoa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta...

WANANCHI LONGIDO WATAKA SHULE ZA BWENI KUIMARISHWA ULINZI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:12

Wananchi wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha wameiomba serikali kujengea uzio shule zote za serikali za bweni zilizopo katika wilaya hiyo lengo ni...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément