SHIRIKA la Grumeti Fund kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii limejivunia mafanikio yake katika kutoa elimu ya kijinsia kwa vijana wa kike na wa kiume...
Vous n'êtes pas connecté
Wanawake kutoka jamii ya kimaasai katika Tarafa ya Longido wilaya ya Longido mkoa wa Arusha wameonyesha furaha yao baada ya shirika la Legal Services Facility (LSF) kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao.Shirika hilo limewawezesha wanawake hao Kwa kuwapatia elimu ya haki za binadamu, haki ya kushiriki katika siasa, afya pamoja na elimu Kwa watoto wa kike.Akizungumza kwenye kigoda cha mwanawake katika wiki ya AZAKI wilayani humo, Mkurugenzi wa LSF Lulu Mwakilala amesema shirika hilo linahakikisha kuwa watu wote wanapata haki sawa hasa wanawake na watoto wa kike."LSF tunashirikiana na serikali kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya juu ili kuhakikisha kuwakuwepo na usawa kati ya mwanamke na mwanaume katika jamii" amesema Mwakilala.Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Longido Upendo Ndorosi amesema kwa sasa kuna mwitikio wa wanawake kushiriki kwenye siasa tofauti na hapo nyuma wakati anagombe nafasi aliyonayo.Anasema changamoto hiyo ilitokana na mfumo dume uliokuwepo ambao shirika la LSF limesaidia kutoa elimu ambayo imeondoa dhana hiyo na sasa hali inaridhisha kidogo."Elimu inayotolewa na mashirika ya kiraia yamewasaidia sana wanawake kupata ujasiri ambapo mpaka sasa katika wilaya hii kuna wanawake kumi na moja ambao nimewashawishi ili wagombee kwenye uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu" amesema Ndorosi.Nabore Nabak ambaye ni Mwenyekiti wa vikundi zaidi ya 300 vya maendeleo wilaya ya Longido amesema wanawake katika wilaya hiyo wanapitia changamoto kadhaa katika harakati za kutafuta usawa."Lakini kupitia vikundi hivi inaonyesha kuwa mwanamke wameelimika na wameionyesha jamii kuwa wanaweza wakaongoza huku akitimiza majukumu yake ya nyumbani" amesema Nabak.Hata hivyo kwa upande wake kiongozi wa mila Laigwanani Lucas Sambeke amesema kwa sasa kupitia vikao vyao vya mila wamekuwa na agenda ya kumuinua mwanamke na mtoto wa kike baada ya kuona matokeo chanya kutoka kwa wanawake."Mila zetu zilikuwa zinamkandamiza mwanamke, lakini tumefanikiwa kwa Asilimia kubwa kushawishi wazee wengine wa mila kupitia sherehe na vikao Ili kuruhusu mwanamke aweze kufanya shughuli za uongozi" amesema Laigwanani Sambeke.
SHIRIKA la Grumeti Fund kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii limejivunia mafanikio yake katika kutoa elimu ya kijinsia kwa vijana wa kike na wa kiume...
Na WMJJWM-DodomaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewataka wadau wanaotoa elimu ya...
Na Mwandishi wetu, KilimanjaroTume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika kuhakikisha inatoa Elimu ya Mpiga Kura kwa makundi mbalimbali katika jamii,...
Imeelezwa kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umepeleka umeme kwa wananchi wapatao 2,400 wa vijiji nane (8) vya Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya...
Na Happiness Shayo- ArushaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka Makamanda wa Kanda na Wahifadhi Wakuu wa...
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya mafunzo ya uongozi kwa wanawake wagombea Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa vijiji, mitaa na vitongoji ...
Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Dodoma Mjini kimeanza mikutano ya ndani ya kuwajengea uwezo wenyeviti wa mashina(Mabalozi) kuelekea Uchaguzi wa...
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi MaryPrisca Mahundi (Mb), amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia...
Na : Jusline Marco;ArushaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu upatikanaji wa...
Na. Elimu ya Afya kwa UmmaKatika kuhakikisha huduma za chanjo zinafanikiwa kwa ufasaha na kuleta tija katika jamii, Manispaa ya Moshi Mkoani...