X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 12/Sep 06:22

WANAWAKE LONGIDO WAJENGEWA UWEZO KUTAMBUA HAKI ZAO

 Wanawake kutoka jamii ya kimaasai katika Tarafa ya Longido wilaya ya Longido mkoa wa Arusha wameonyesha furaha yao baada ya shirika la Legal Services Facility (LSF) kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao.Shirika hilo limewawezesha wanawake hao Kwa kuwapatia elimu ya haki za binadamu, haki ya kushiriki katika siasa, afya pamoja na elimu Kwa watoto wa kike.Akizungumza kwenye kigoda cha mwanawake katika wiki ya AZAKI wilayani humo, Mkurugenzi wa LSF Lulu Mwakilala amesema shirika hilo linahakikisha kuwa watu wote wanapata haki sawa hasa wanawake na watoto wa kike."LSF tunashirikiana na serikali kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya juu ili kuhakikisha kuwakuwepo na usawa kati ya mwanamke na mwanaume katika jamii" amesema Mwakilala.Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Longido Upendo Ndorosi amesema kwa sasa kuna mwitikio wa wanawake kushiriki kwenye siasa tofauti na hapo nyuma wakati anagombe nafasi aliyonayo.Anasema changamoto hiyo ilitokana na mfumo dume uliokuwepo ambao shirika la LSF limesaidia kutoa elimu ambayo imeondoa dhana hiyo na sasa hali inaridhisha kidogo."Elimu inayotolewa na mashirika ya kiraia yamewasaidia sana wanawake kupata ujasiri ambapo mpaka sasa katika wilaya hii kuna wanawake kumi na moja ambao nimewashawishi ili wagombee kwenye uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu" amesema Ndorosi.Nabore Nabak ambaye ni Mwenyekiti wa vikundi zaidi ya 300 vya maendeleo wilaya ya Longido amesema wanawake katika wilaya hiyo wanapitia changamoto kadhaa katika harakati za kutafuta usawa."Lakini kupitia vikundi hivi inaonyesha kuwa mwanamke wameelimika na wameionyesha jamii kuwa wanaweza wakaongoza huku akitimiza majukumu yake ya nyumbani" amesema Nabak.Hata hivyo kwa upande wake kiongozi wa mila Laigwanani Lucas Sambeke amesema kwa sasa kupitia vikao vyao vya mila wamekuwa na agenda ya kumuinua mwanamke na mtoto wa kike baada ya kuona matokeo chanya kutoka kwa wanawake."Mila zetu zilikuwa zinamkandamiza mwanamke, lakini tumefanikiwa kwa Asilimia kubwa kushawishi wazee wengine wa mila  kupitia sherehe na vikao Ili kuruhusu mwanamke aweze kufanya shughuli za uongozi" amesema Laigwanani Sambeke.

Articles similaires

MAIPAC KUJA NA MKAKATI WA KUELIMISHA MADHARA YA UKEKETAJI

msumbanews.co.tz - 13/Sep 06:08

 LSF nao kuendelea kusaidia vikundi wanawake Longido.Shirika la Wanahabari la usaidizi wa.jamii za pembezoni(MAIPAC) linatajia  kuzindua mradi...

MAIPAC KUJA NA MKAKATI WA KUELIMISHA MADHARA YA UKEKETAJI

msumbanews.co.tz - 13/Sep 06:08

 LSF nao kuendelea kusaidia vikundi wanawake Longido.Shirika la Wanahabari la usaidizi wa.jamii za pembezoni(MAIPAC) linatajia  kuzindua mradi...

WATUMIA SHEREHE ZA UBATIZO KUKEKETA WATOTO SERIKALI YAONYA

msumbanews.co.tz - 17/Sep 09:34

Baadhi ya familia za Jamii ya kimasai wilaya ya Longido mkoa Arusha,zinadaiwa kutumia sherehe za Ubalozi kukeketa watoto wadogo ili kukwepa kukamatwa...

MAIPAC KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE KUTETEA HAKI ZAO

msumbanews.co.tz - 12/Sep 10:31

 MAIPAC kuzindua mradi wa kuelimisha ukeketaji kwa watoto wa kike katika jamii ya kifugaji ya kimasai ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanawake uwezo wa...

MAIPAC KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE KUTETEA HAKI ZAO

msumbanews.co.tz - 12/Sep 10:31

 MAIPAC kuzindua mradi wa kuelimisha ukeketaji kwa watoto wa kike katika jamii ya kifugaji ya kimasai ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanawake uwezo wa...

DKT. KIRUSWA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUMTUMBUA ALIYEKUWA DC LONGIDO

msumbanews.co.tz - 06/Sep 17:10

 Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoani Arusha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Lemomo Kiruswa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa...

WIKI YA AZAKI KUHAMASISHA JAMII KUSHIRIKI DIRA 2050, UCHAGUZI

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:02

 Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society FCS- Justice Rutenge, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini...

DKT. KIRUSWA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA UTOAJI HUDUMA MGODINI

msumbanews.co.tz - 07:00

 Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameshuhudia Utiaji Saini wa Mikataba ya usambazaji na utoaji wa huduma mgodini katika mgodi wa uchimbaji...

SERIKALINI YAKEMEA UCHAFU WA MASHUKA HOSPITALINI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 10:16

Serikali imesema kuwa itaanza kuchukua hatua kwa wahudumu wa afya watakaobainika kuzembea katika usafi na kusababisha mashuka ya vitanda vya wagonjwa...

SERIKALINI YAKEMEA UCHAFU WA MASHUKA HOSPITALINI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 10:16

Serikali imesema kuwa itaanza kuchukua hatua kwa wahudumu wa afya watakaobainika kuzembea katika usafi na kusababisha mashuka ya vitanda vya wagonjwa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément