X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 13/Sep 05:34

ZAIDI YA BILIONI 19 KUTEKELEZA MRADI WA UMEME VITONGOJINI MWANZA

 MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi Bilioni 19 kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Umeme kwenye vitongoji 135 Mkoani humo katika majimbo yote tisa.Ametoa pongezi hizo leo Septemba 12, 2024 ofisini kwake wakati akizungumza na Ujumbe wa wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliomtembelea wakiongozana na Cylex Engineering Company ambaye ndie mkandarasi wa mradi.Amesema Mhe. Rais anaendelea kuboresha maisha ya wananchi wake kwa kasi ndio maana amemaliza kuweka huduma za umeme kwenye vijiji vyote nchini na sasa anaelekeza nguvu kwenye vitongoji kwa kuhakikisha wanapata Nishati Safi.Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa Wakala kumsimamia Mkandarasi vema ili akamilishe mradi kwa wakati kwa mujibu wa mkataba ili kwa haraka huduma za umeme ziweze kuwafikia wananchi.Vilevile, amemtaka mkandarasi huyo kutumia wananchi wazawa kwenye maeneo ya mradi katika ajira ndogondogo zitakazotolewa na kuhakikisha wanawalipa kwa wakati ili kuepusha migogoro isiyo lazima kwenye eneo la kazi.Akizungumzia upatikanaji wa huduma ya umeme Mhe. Mtanda amesema Mwanza ina nishati ya kutosha kwani ni megawati 86 pekee zinatumika kwa sasa pamoja na kuzalishwa zaidi ya megawati 100 hivyo kumekua na ziada ambayo itatumika pindi miradi ya kimkakati itakapoanza.Awali, Msimamizi wa miradi ya Wakala wa Nishati vijijini REA Kanda ya ziwa Mhandisi Ernest Makale amesema mradi huo kwenye vitongoji unadhihirisha na kubainisha nia ya serikali ya kuhakikisha kila kitongoji nchini kinakua na umeme ifikapo 2030.

Articles similaires

ZAIDI YA BILIONI 19 KUTEKELEZA MRADI WA UMEME VITONGOJINI MWANZA

msumbanews.co.tz - 13/Sep 05:34

 MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi Bilioni 19 kwa ajili ya...

REA YAENDELEA KUTEKELEZA DHAMIRA YA RAIS SAMIA KWA VITENDO

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:03

Na Mohamed SaifWakala wa Nishati Vijijini (REA) umeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la...

WIZARA YA NISHATI ENDELEENI KUUSIMAMIA MRADI WA JNHPP IPASAVYO-KAMATI YA BUNGE

msumbanews.co.tz - 07/Sep 15:39

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeitaka Wizara ya Nishati kuendelea kuusimamia ipasavyo Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Julius Nyerere...

JKT YASAINI MKATABA NA REA KUWEZESHA MRADI WA KUFUNGA MIFUMO YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

msumbanews.co.tz - 14/Sep 05:42

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy,...

SERIKALI KUVUTIA WAWEKEZAJI UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI- DKT. BITEKO

msumbanews.co.tz - 10/Sep 16:13

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali itaendelea kuvutia wawekezaji katika tafiti na uchimbaji wa mafuta na...

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA FEDHA ZA MIRADI YA REGROW

msumbanews.co.tz - 08/Sep 05:38

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ikiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb)imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa...

DKT.JAFO AAGIZA  MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KILWA KUKAMILIKA KWA WAKATI

msumbanews.co.tz - 08:28

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa...

WAZIRI JAFO ATAKA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KILWA KUKAMILIKA KWA WAKATI

msumbanews.co.tz - 10:27

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa...

WAZIRI JAFO ATAKA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KILWA KUKAMILIKA KWA WAKATI

msumbanews.co.tz - 10:27

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa...

Dc Ilala awataka Viongozi wa Matawi, Mashina, Mitaa na Kata kutimiza majukumu yao kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

msumbanews.co.tz - 15/Sep 05:19

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Mhe. Edward Mpogolo amewataka Viongozi wa Matawi, Mashina, Mitaa na Kata  Kutimiza Majukumu yao kuelekea Uchaguzi wa...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément