X

Vous n'êtes pas connecté

Rubriques :

Maroc Maroc - MSUMBANEWS.CO.TZ - A La Une - 13/Sep 05:24

WATANZANIA ASILIMIA 80 KUFIKIWA NA ELIMU YA FEDHA

 Na. Saidina Msangi, Kibaha, Pwani.Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau na Taasisi zilizo chini yake imejipanga kutoa elimu ya fedha kwa Watanzania asilimia 80 ifikapo mwaka 2025 ili wawezesha wananchi kufahamu umuhimu wa akiba, bima, usimamizi wa fedha binafsi pamoja na kutumia watoa huduma rasmi wa fedha waliosajiliwa.Hayo yamebainishwa na Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha m, Bw. Stanley Kibakaya, wakati wa kuhitimisha programu ya utoaji wa elimu ya fedha kwa wananchi katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.Alisema kuwa elimu hiyo ya fedha imepokelewa vizuri na wananchi katika mikoa ya Kagera, Manyara, Singida, Kigoma, Rukwa, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Mtwara, Morogoro, Lindi na mikoa mingine inatarajiwa kufikiwa katika awamu ijayo. ‘‘Tunafanyia kazi maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa Wizara ya Fedha kuendelea kutoa elimu ya fedha kwa wananchi na pia mpango wa sekta ya fedha unalenga kutoa elimu ya fedha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia taasisi za fedha zilizosajiliwa wanapochukua mikopo ili kuwawezesha kuondokana na mikopo umiza,’’alisema Bw. Kibakaya.Alisema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa elimu ya fedha na wananchi wameifurahia na kukiri kuwa elimu hiyo imewasaidia na wataenda kuzitumia huduma rasmi za fedha ikiwemo kuweka akiba, uwekezaji na bima.Kwa upande wao wananchi wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani, wameipongeza Serikali kwa kuwapatia elimu hiyo muhimu ambayo wanaeleza kuwa itawawezesha kujikwamua kiuchumi pamoja na kujiandaa kutumia fursa za uwekezaji katika mifumo rasmi ikiwemo UTT AMIS.

Articles similaires

WIZARA YA FEDHA YAKEMEA MIKOPO HOLELA YA MITAANI INAYODHALILISHA WATANZANIA

msumbanews.co.tz - 12/Sep 07:52

 Na Mwamvua Mwinyi,KibahaWIZARA ya fedha imetoa rai kwa Watanzania hususan makundi ya akinamama na wajasiriamali kujiepusha na mikopo ya...

ELIMU YA FEDHA YAWAFIKIA WANANCHI WA MKURANGA

msumbanews.co.tz - 11/Sep 05:10

 Na. Saidina Msangi, Mkuranga Pwani.Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, imewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa...

WANANCHI CHALINZE WAJIPANGA KUWEKEZA

msumbanews.co.tz - 07/Sep 07:41

 Na. Saidina Msangi, Chalinze, Pwani.Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia elimu ya fedha...

WANANCHI BAGAMOYO WAPOKEA ELIMU YA FEDHA

msumbanews.co.tz - 09/Sep 07:12

 Na. Saidina Msangi, WF, Bagamoyo, Pwani.Watumishi na wananchi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wameishukuru Serikali kwa kuwapa mafunzo ya elimu...

DKT. BITEKO AHIMIZA WANAWAKE KUTUMIA MIFUKO YA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

msumbanews.co.tz - 14/Sep 13:14

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanawake nchini kutumia fursa ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi...

WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO KWA MAAFISA UNUNUZI WA TAASISI ZA UMMA.

msumbanews.co.tz - 06/Sep 04:51

 Na Chedaiwe Msuya, WF.Wizara ya Fedha inaendelea kutoa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta...

MAAFISA UNUNUZI WA UMMA WAASWA KUFUATA SHERIA.

msumbanews.co.tz - 05/Sep 06:14

 Na Asia Singano, WF- KilimanjaroMaafisa Ununuzi wa Umma nchini wametakiwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Ununuzi wa Umma ili kufikia malengo...

WIZARA YA FEDHA IMEHITIMISHA KUTOA MAFUNZO YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA KANDA YA KUSINI

msumbanews.co.tz - 07/Sep 11:55

 Na Chedaiwe Msuya,WFWizara  ya Fedha imehitimisha utoaji wa mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi kwa Umma  katika mikoa ya Mtwara, Lindi na...

NG'UMBI AWATAKA WADAU KUONGEZA USHIRIKIANO KATIKA ELIMU

msumbanews.co.tz - 16:38

Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Michael Ng’umbi akifafanua jambo wakati wa mahojiano maalum kuhusu hali ya elimu nchini kupitia...

WAZIRI JAFO ATAKA WATANZANIA KUJIAMINI NA KUWEKEZA KATIKA VIWANDA NCHINI

msumbanews.co.tz - 12/Sep 05:54

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) akioneshwa na Mkurugenzi wa Hill Group Bw. Hillary Shoo jinsi mchakato wa uzalishaji nyama...

Les derniers communiqués

  • Aucun élément