Na Veronica Simba, WMA DodomaWakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Dodoma imetoa elimu ya vipimo kwa Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa...
Vous n'êtes pas connecté
Na Pendo Magambo – WMA, Dar es SalaamWakala wa Vipimo Tanzania (WMA) imewataka wafanyabiashara wa gesi kutumia mizani iliyohakikiwa na WMA ili kujiridhisha na usahihi wa uzito wa mitungi ya gesi kabla ya kuiuza kwa wateja.Wito huo ulitolewa Septemba 3, 2024 jijini Dar es Salaam na Afisa Vipimo Yahya Tunda kutoka WMA Mkoa wa kivipimo Ilala, wakati wa semina jumuishi iliyoandaliwa na kampuni ya Gesi ya Oryx kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wote.Tunda alieleza kuwa WMA inatekeleza majukumu yake kupitia Sheria ya Vipimo sura namba 340, ambayo inasimamia matumizi ya vipimo sahihi na kwa upande wa wafanyabiashara wanaotumia mizani, sheria inawataka kutumia zile zilizohakikiwa na WMA ili kuleta usawa wa kivipimo kwenye maeneo ya biashara, afya, usalama na mazingira.“Ninawashauri wafanyabiashara pindi wanapotaka kununua mizani kufika katika ofisi zetu ili wapate ushauri wa kitaalamu kuhusu aina inayofaa kulingana na biashara wanazofanya,” alisisitiza.Akizungumzia kuhusu mizani inayotumiwa na wafanyabiashara kuhakiki uzito wa bidhaa, Tunda alisema kuwa sheria inaelekeza kuweka kibandiko kinachoonesha tarehe ambayo mizani ilihakikiwa pamoja na tarehe ya kurudia uhakiki wake.Aidha, aliwataka wafanyabiashara wa gesi walioshiriki semina hiyo kuwa mabalozi kwa wengine.Kwa upande wake, Msimamizi wa kampuni ya Oryx, Wilaya ya Ilala, Evarist Kisaka aliishukuru WMA kwa kuitikia wito na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa wafanyabiashara wa gesi na wadau mbalimbali wa nishati safi ya kupikia.“Waliohudhuria leo wamepata maarifa mengi, nina uhakika wataenda kufanya biashara zao kwa mlengo chanya zaidi maana wamejua faida za kuwa na vipimo sahihi, suala ambalo litawajengea uaminifu kwa wateja,” alisema.Pamoja na jukumu lake la msingi ambalo ni kumlinda mlaji na mfanyabiashara, WMA pia inachagiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wote kwa kuhakikisha kuwa panakuwa na usawa katika vipimo vya bidhaa hiyo yanayoendana na thamani ya fedha katika biashara husika.
Na Veronica Simba, WMA DodomaWakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Dodoma imetoa elimu ya vipimo kwa Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa...
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amehimiza wananchi jijini Mwanza kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo kila mara wanapofanya...
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Septemba...
Na Mahamudu Jamal, WMAWakala wa Vipimo (WMA) imekabidhi msaada wa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Jeshi la Polisi Mkoa...
Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali inaendelea kutekeleza mkakati wa nishati safi ya kupikia utakaowafanya watanzania zaidi ya...
Na Mohamed SaifWakala wa Nishati Vijijini (REA) umeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la...
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Alban Kihulla akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari katikq Mkutano mwendelezo ya Mikutano...
Na. Benny MwaipajaWaziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ((Mb), ametoa wito kwa nchi za Afrika kutafuta njia na mikakati ya kuboresha...
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali itaendelea kuvutia wawekezaji katika tafiti na uchimbaji wa mafuta na...